Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema jumla ya watu 26 ndiyo waliokolewa kati ya 43 waliokuwa ndege ya Precion Air iliyokuwa ikijiandaa kutua Bukoba na kwamba wote walipelekwa walipelekwa katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera huku wananchi wakimpongeza rubani kwa uamuzi sahihi.
Waliookolewa walipelekwa Hospitalini kwa ajili ya uangalizi, baada ya ndege kupata ajali na kutua ziwani ikidaiwa kuwa huo ni uamuzi sahihi wa Rubani kwani kama ingetua ardhini maafa yangekuwa makubwa na watu hao waliokolewa kabla sehemu kubwa ya ndege haijazama kwenye maji, huku Mkuu huyo wa Mkoa akisema wataendelea kutoa taarifa kila baada ya muda.
Kufuatia ajali hiyo na shughuli za uoakoaji zinavyoendelea, Chalamila amewaomba Wananchi kuwa watulivu wakati taratibu zingine zikifanyika na kwamba bado hakuna taarifa za kifo na mawasiliano kwa kila idara yanaendelea vyema.
Ndege hiyo aina ya ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF, ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikua irudi Dar es Salaam kupitia Mkoa wa Mwanza.