Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dkt. Issessanda Kaniki amethibitisha kupokea miili ya watu watatu waliofariki Dunia katika ajali ya Ndege, iliyotokea mapema Asubuhi ya Leo.
Dkt. Kaniki amesema jitihada za kuwapatia matibabu watu wengine zinaendelea katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, huku hali za majeruhi zikizidi kuimarika.
Kutokana na ajali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kufika Mkoani humo muda wowote kuanzia sasa.
Ndege hiyo aina ya ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF, mali ya Precision Air ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikua irudi Dar es Salaam kupitia Mkoa wa Mwanza.