Ndege ya jeshi la wananchi wa Tanzania yenye usajili namba JW 9127, iliyokuwa imebeba marubani wawili wa kijeshi imepata ajali leo Julai 20, 2023 wakati ilipokuwa ikijaribu kutua kwa dharula katika uwanja wa ndege wa Bukoba.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Blasius Chatanda amesema hakuna kifo katika jali hiyo na Makamanda hao Meja Leonard Levokatus (45) na Luten Alex Venance (30) wanaendelea vizuri kiafya na tayari wamesharuhusiwa.

Amesema, “Ndege hiyo ambayo ilitua hapa kwa dharula ulikuwa katika mafunzo yanaayoendelea kwa wanajeshi hawa kwa ujumla hali za marubani ni shwari, hatuna majeruhi lakini pia hatuna kifo na wameangaliwa na wataalam wa afya na wameruhusiwa.”

Hata hivyo ameongeza kuwa, chanzo cha ajali bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea ambao utashirikisha mamlaka tofauti tofauti ili tuweze kupata uhakika wa nini kilisababisha huku Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Erasto Sima akilipongeza JWTZ na Zimamoto na uokoaji kwa kufika kwa wakati na wadau kujitokeza kutoa msaada.

BUWSSA yaweka mkakati kuondoa upotevu wa maji
Mamlaka Wakuu wa Mikoa, Wilaya yanatumika vibaya