Wananchi wametolewa hofu kwamba hakukuwa na ajali ya Ndege iliyotekea Mkoani Mtwara, bali lilikuwa ni zoezi la utayari lililofanywa na uongozi wa kiwanja cha ndege cha Mtwara kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas akiwa kiwanjani hapo, na kudai kuwa kumekuwepo na taharuki miongoni mwa jamii lakini hakuna madhara isipokuwa ni zoezi la utayari.
Amesema, “wakati nakuja hapa nilikua najiuliza nchi hii tena ikoje, tumetoka Hanang’ sasa tunahamia Mtwara, kidogo nilipata simanzi, lakini mwisho nimekuja kubaini kumbe ni zoezi na mimi nichukue fursa hii kumshkuru Mwenyezi Mungu kuepusha na tatizo hilo.”
Awali, Meneja wa Kiwanja cha Ndege Mtwara, Jordan Mchami katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa alisema zoezi hilo ni sehemu ya miongozo ya uendeshaji wa Viwanja vya Ndege Kitaifa na Kimataifa na kwamba wanatakiwa kulitekeleza kila baada ya miaka Miwili.