Mkoa wa Rukwa Wilayani Sumbawanga watu watatu wakazi wa Kitongoji cha katandala wa familia moja akiwemo baba, mama na mtoto wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyohusisha pikipiki na basi la Kampuni ya Saratoga.
Waliofariki katika ajali hiyo ya kusikitisha ni Chrispin Senga mwenye umri wa miaka 40, Salome Chaulinge mwenye umri wa miaka 31 na Mtoto wao Paulina Senga wa miaka
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema tukio hilo limetokea leo, Mei 29 saa 6 mchana katika eneo la kituo cha mafuta cha Munio, mjini hapa.
Kamanda Kyando amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Saratoga lenye namba T 211 AED aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Ally Fabiano (31) mkazi wa Kigoma.
-
Lukuvi afikisha ujumbe mzito kwa wamiliki wa ardhi
-
Nape ampa mkono Kinana, aikumbuka mbegu aliyopanda
“Basi hilo lilikuwa likitokea Sumbawanga mjini kuelekea mkoani Kigoma na wanafamilia hao walikuwa wamepanda pikipiki yao aliyokuwa akiendesha Senga,” amesema Kyando.
Kamanda wa polisi amesema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea ilikuwa vigumu kuitambua miili ya wazazi kwani iliharibika vibaya ila kichwa cha mtoto peke yake ndio kilionekana.
“Ilikuwa vigumu hata kuitambua miili ya wale wazazi wa mtoto paulina kwani aliharibika vibaya lakini mtoto peke yake ndio kichwa kilionekana.” amesema Kyando.