Watu kumi wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya ajali ya gari kutokea Same, mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Makanya nje kidogo ya mji wa Same mkoani humo ambapo gari aina ya Toyota Alphard limegongana na Hiace.

Mkuu wa Wilaya hiyo,Rosemary Senyamule amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana Aprili 13,2021.

Kufuatia ajali hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole na rambirambi kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika “Nimesikitishwa na taarifa ya vifo vya watu 10, waliofariki dunia katika ajali ya gari huko Same Mkoani Kilimanjaro. Nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wapone haraka. Aidha, nawasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali.”

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 14, 2021
Vipaumbele vya serikali katika utekelezaji mpango wa maendeleo