Watu sita wamefariki na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Kambi ya Jeshi Sopa, Kata ya Meserani Wilaya ya Monduli, Mkoani Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa waa Arusha, Salum Hamduni amesema ajali imetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Padri Sixtus Masawe wa Kanisa Katoliki Parokia ya Masaktas Jimbo la Mbulu, Manyara ni mmoja kati ya waliopoteza maisha.

Imeelezwa, ajali ilitokea baada ya gari aina ya Toyota Hardtop mali ya Jimbo la Mbulu kugonga lori lililokuwa limeharibika.

Dereva wa gari hilo Francis Gitayane ni miongoni mwa majeruhi waliolazwa Hospitali ya Mount Meru.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 27, 2020
Andre Villas-Boas: Jezi namba 10 istaafishwe

Comments

comments