Watu nane wamefariki na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea mjini Bukoba mkoani Kagera ikihusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace linalofanya safari zake kati ya Kemondo na Bukoba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo amesema ajali hiyo  imetokea Novemba 22, majiraya saa 1: 40 usiku atika Barabara ya Uganda eneo la Rwamishenye Manispaa ya Bukoba.

Kwa mujibu wa Kamanda Mulimi katika watu waliopoteza maisha , watano walipoteza maisha palepale, kati yao watatu wakiwa ni abiria wa gari hilo, na  wawili walikuwa ni watembea kwa miguu ambao waligongwa wakati gari hilo lilipopoteza mwelekeo.

Kamanda Mulimi ameeleza kuwa mmoja alifia mapokezi Hospitali ya Rufaa ya Bukoba na majeruhi wawili walipoteza maisha wakati  wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo na kufanya idadi ya waliofariki kuwa nane.

Kwa mujibu wa Polisi hadi sasa chanzo  cha ajali hakijafahamika, bado kinachunguzwa  ingawa Kamanda Mulimi amesema kuwa “Ukingalia kwa jicho la kawaida, na matokeo ya uharibifu wa chombo cha usafiri ni dhahiri ajali hiyo imechangiwa na mwendokasi.”

Kaze kufanya mabadiliko Young Africans
Kocha Morocco aifikiria Al Rabita FC

Comments

comments