Kiungo Mshambuliaji Wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa sababu kubwa ya kutokuwa kwenye kikosi cha kwanza ni matatizo ya kifamilia.
Ajibu ameweka wazi kuwa awali chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroec alikuwa na nafasi kikosi cha kwanza ila mambo yalibadilika alipopata matatizo.
“Nimecheza mechi nyingi kuliko zile nilizokaa benchi tangu aje kocha huyu ndani ya Simba,(Sven).
“Mwanangu aliumwa na kulazwa hospitali sikusafiri na timu nikawa namuhangahikia yeye na hapo wenzangu wakaenda kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na Lipuli kule Iringa.
“Inafahamika kuwa tumu inayoshinda haibadilishwi ndiyo maana nikakosa nafasi lakini tangu kocha kaja nina nafasi ila imetokea tu,” amesema.
Ajibu amefunga bao moja kati ya mabao 63 yalifungwa na Simba huku akitoa pasi nne za mabao.