Kijana mmoja kutoka nchini Australia ambaye jina lake halikutajwa kwasababu za kisheria amekiri kuudukua mtandao wa Apple na kuiba nyaraka kadhaa za mtandao huo huku akiwa na lengo la kufanya kazi na kampuni hiyo.
Kijana huyo wa kiume mwenye miaka 16 aliingia kwenye mtandao huo mara kadhaa mwaka huu kutoka nyumbani kwao Melbourne, Australia kwa mujibu wa gazeti la Age,
Amesema kuwa alihifadhi nyaraka hizo kwenye ghala linalofahamika kama ‘hacky hack hack’, huku kampuni ya Apple ikisema kuwa hakuna taarifa za wateja wake zilizovuja.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa mahakamani, kampuni ya simu ililijulisha shirika la ujasasi la Marekani baada ya kupata taarifa za udukuzi huo na kuwajulisha polisi wa Australia AFP.
-
Mapadri wakumbwa na kashfa ya udhalilishaji wa kingono Marekani
-
Marekani yadai China inajiandaa kuishambulia kijeshi
-
Umoja wa Ulaya wainyooshea kidole Uganda
Hata hivyo, gazeti la Age limeripoti kuwa alidukua kwa sababu alikuwa shabiki mkubwa wa Apple na alikuwa na ndoto ya kufanya kazi huko, huku wakili wake akisema kuwa kijana huyo amejichukulia umaarufu mkubwa kwa jamii ya wadukuzi duniani.