Williamu Mwalugelo (46) mkazi wa Kawajense Manispaa ya Mpanda amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila kwa kujining’iniza kwenye dari chumbani kwake akituwatuhumu wajomba zake wawili kuua ndugu zake 16 kwa njia za ushirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Ambapo amesma kabla ya hapo marehemu alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kusababisha taharuki katika eneo la Mpandahoteli kutokana na vitu alivyokuwa amebeba vinavyoashiria ushirikina. 

“Kweli tulimkamata tulipigiwa simu na wajomba zake amepeleka vitu vya kishirikina, aliwekewa dhamana, siku ya kupelekwa mahakamani aliomba ruhusa afuate mdhamana akaenda kujinyonga,” amesema Makame.

Lusinde: Mawaziri jihadharini na Dkt Tulia
Waandamanaji wawili wauawa Sudan wakati wa maandamano