Kitachana Shenani (30), mkazi wa kitongoji cha Senta kijiji cha Makundusi Wilaya ya Serengeti amejijyonga kwa kamba hadi kufa baada ya kukataliwa na mpenzi wake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu, Katibu Tawala Wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara amesema tukio hilo limetokea Aprili 11 majira ya saa 11 jioni.

Amesema, Shenani alikataliwa na mpenzi wake Pilly Kikono (39) mfanyabiashara ya viatu kijiji cha Natta mbele ya familia kwa madai kuwa amekuwa akimfanyia fujo ikiwemo kumpiga.

Kwa mujibu wa tovuti ya Mwananchi, Kaka wa marehemu Jokonasi Shenani ameeleza kuwa mpenzi wake huyo (Pilly), alimkataa mbele yao kuwa hamtaki atafute mwanamke mwingine.

“Alikuja na nguo zake akatukabidhi na kudai kuwa hataki kumuona tena kwake lakini mdogo wangu akadai hakubaliani na uamuzi huo kwa kuwa anampenda sana na huenda amepata mwingine,” amesema.

Amesema jioni alipata taarifa ya kujinyonga kwake kupitia wachunga mifugo

“Inashangaza sana kwa kuwa familia ilimtaka atafute mke aoe,” amesema.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Makundusi Mseti Nyaikobe amesema, baada ya uchunguzi wa Polisi na Mganga kubaini chanzo cha kifo ni kujinyonga familia imekabidhiwa mwili na taratibu za maziko zinaendelea.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 13, 2021
Mwambusi aahidi mabadiliko Young Africans