Mwanaume mmoja mkoani Rukwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya nailoni baada ya kugundua mkewe ametoroka usiku na kwenda kwa mwanaume mwingine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amesema mnamo novemba 26, 2019 saa 6 usiku, mwanaume iliyefahamika kwa jina la Rafael Leonard (49) mkazi wa kijiji cha Bumanda wilayani Nkasi, alijinyonga chumbani kwake kwa kamba ya nailoni.
Amesema kabla ya kujinyonga alikuwa amelala na mkewe, aliposhtuka usingizini alikuta mke wake ametoroka na kwenda kwa mwanaume mwingine ndipo alipokasirika na kupatwa na wivu wa kimapenzi na kuamua kujinyonga.
Muhimbili yafanya upasuaji wa kurekebisha Jinsi tata
katika tukio jingine, Novemba 23 wilayani humo, watu wawili waliofahamika kwa majina ya Japhet Jelazi (25) na Peter Silunde (8) walipoteza maisha baada ya kupigwa na radi wakiwa wamejikinga mvua chini ya mti.
Aidha kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha mvua za masika ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.