Mkazi wa kijiji cha Gamash wilayani Geita, Paulo Hassan anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya mika 40 anadaiwa kujinyonga na shuka kwa hasira baada ya mkewe kuuza kondoo na kutumia fedha bila kumshirikisha.

Mke wa marehemu, Jenipha Lateremla ameliambia gazeti la mwananchi kuwa mumewe alijinyonga usiku wa kuamkia Januari 18 baada ya kutokea ugomvi baina yao.

Amesema usiku wa kuamkia Januari 17 wakiwa chumbani, mumewe alianza kuhoji alipopeleka kondoo, alipomueleza kuwa alimuuza kwaajili ya maandalizi ya sikuku ya krismasi na fedha tayari alizitumia kwenye sikukuu hiyo mwaka jana ndipo alipoanza kuonesha kukasirika.

“Tukiwa tumelala usiku, akaniambia tena, unajua moyo wangu ulivyo na na hasira, hela umefanyia nini? nilivyoona hivyo kwakuwa akikasirika huwa ananipiga nilitoka nje nikamuacha” amesema Jenipha.

Alipotoka nje mumewe alifunga mlango na mkewe akabaki nje na kuwagongea watoto na asubuhi watoto walipoamka walimgongea baba yao kwaajili ya kumsalimia, lakini hakuitikia na walipochungulia ndani walikuta amejinyonga kwa shuka lake la kulalia.

Diwani wa viti maalumu (CCM) wa Bulela, Salome Kitura amesema kuwa tayari polisi wametoa kibali cha familia kutoa mwili wa marehemu na kuuzika huku akitoa wito kwa wananchi wanapokuwa na hasira wajenge tabia ya kuomba ushauri.

Wanawake U -20 washusha kipigo Uganda
Video: TCRA - Tunazima laini zisizosajiliwa, Wengi waachwa

Comments

comments