Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mtongani amejinyonga hadi kufa nyumbani kwao baada ya Mama yake mzazi kumtuhumu kuiba Shilingi 5,000.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo limetokea Mei 24, 2021 na uchunguzi umebaini kilichopelekea kifo cha mtoto huyo wa miaka 14 ni tuhuma za kuiba fedha hiyo.

Jeshi la Polisi Mkoa inamshikilia Mama pamoja na Baba Mlezi huku mahojiano zaidi yakifanyika.

Manara atuma ujumbe mzito mitandaoni
Watu 6 mbaroni kwa tuhuma kufukua mwili wa marehemu