Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Madirisha Kanyalu (60) amejiua kwa kujitumbukiza kwenye kisima baada ya kumuua mtoto wake Meshack Madirisha (miezi 11) pamoja na mkewe aitwaye Evodia Nyerere (27) kwa kutumia kitu chenye makali akimtuhumu mkewe kuchepuka na wanaume wengine.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul tukio hilo limetokea Machi 2,2022 majira ya saa 12 asubuhi katika maeneo ya kitongoji cha Mwamadulu kijiji cha Bulambila kata ya Mwalukwa wilaya ya Shinyanga.

Amesema kuwa Mtuhumiwa Madirisha Kanyalu alitoroka baada ya tukio na kwenda kujitumbukiza kwenye kisima cha maji kilichopo karibu na nyumba yake aliyokuwa anaishi na kufariki dunia.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia ambapo Madirisha Kanyalu alikuwa anamtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya wanaume wengine

Breaking News: Mbowe akutana na Rais Samia Ikulu usiku huu
Wanawake wapewa kipaombele kwenye sensa