Bibi wa miaka 74, Yerramatti Raja raia wa India amebahatika kujifungua watoto wakike mapacha baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka 54 bila kupata mtoto na daktari amethibitisha kuwa bibi huyo amejifungua salama na anaendelea vizuri.

Hata hivyo wazazi waliomsaidia kumzalisha bibi huyo wamesema amejifungua kwa njia ya kuanguliwa mayai yake ya uzazi nje ya mfuko wa uzazi na baadaye kuchanganywa na mbegu za kiume na kisha kupandikizwa ndani ya mfuko wake wa uzazi kwa lugha ya kitaalamu inaitwa IVF.

Mwanamke huyo amesema yeye na mumewe  mwenye umri wa miaka 82 walikuwa wakitaka kuwa na watoto katika kipindi chao chote cha ndoa lakini ilishindikana.

Kitaalamu mwanaume anauwezo wa kutungusha mimba hata katika umri wa uzee tofauti na mwanamke  ambaye kadri anapokaribia utu uzima ndipo anapoanza kupoteza uwezo wa kushika ujauzito kutokana na sababu za kiumri.

Na wanawake wengi huanza kupoteza uwezo wa kuzaa kuanzia umri wa miaka 40 hadi 50 na kuendelea.

Hivyo kitendo cha mwanamke huyo kuweza kupata  watoto katika umri huo wa uzee ni jambo la ajabu kwani walikuwa ni watu waloihisi kutengwa na jamii na wanakijiji wenzake na mara kwa mara alikuwa akitengwa katika mikusanyiko kwa sababu ya kutokuwa mama.

‘’Walikuwa wananiita mwanamke asiye na mtoto, tulijaribu mara nyingi kupata watoto na tuliwatembelea madaktari wengi kwahiyo hiki ni kipindi cha furaha zaidi maishani mwetu”amesema Yerramatti Raja

Aidha pacha hao wawili wakike walizaliwa kwa njia ya upasuaji jambo ambalo ni nadra.

Tukio kama hilo limewahi kutokea tena nchini India ambapo mwanamke wa umri wa miaka 70 Daljinder Kaur alijifungua mtoto wa kike.

 

Sudan yarudishiwa uanachama AU
Vurugu Afrika Kusini zamvuta Rais wa Nigeria, kufanya ziara