Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 50 anayefahamika kama mtumishi wa Mungu wa imani ya dini ya Kiislam amekamatwa pamoja na mwanae wa kike kwa tuhuma za kuwapa ombaomba wanaokaa karibu na msikiti maandazi yenye sumu nchini Nigeria.

Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Mohammed Yusuf na mwanae Salamat (18), walifikishwa katika mahakamani jijini Lagos, wakikabiliwa na mashtaka ya jaribio la kuua na njama ya kudhuru, waliyodaiwa kuyafanya August 5 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika mitaa ya Offin, Balogun, Lagos.

Mwendesha mashtaka, Ben Ekundayo aliieleza mahakama ya Lagos kuwa washtakiwa walitekeleza makossa hayo kwa nia ya kutaka kudhuru maisha ya ombaomba hao.

“Muhamad Yusuf alimtuma mwanae kuwapa ombaomba mikate/maandazi karibu na msikiti, lakini mmoja kati ya ombaomba hao alipasua katikati na kugundua kuna vitu kama sindano ndogo, ndipo alipowashtua wenzao ambao pia waligundua kuna kitu kilichowekwa ndani,” mwendesha mashtaka alieleza.

“Mmoja wao ambaye alikuwa anafahamu shule anayosoma binti aliyewapa chakula hicho aliwapeleka wenzake pamoja na polisi na wakafanikiwa kumkamata na kisha aliwapeleka kwa baba yake,” aliongeza.

Hata hivyo, washtakiwa wote walikana mashataka yote dhidi yao.

Hakimu, Ade Adefulire alitoa masharti ya dhamana kwa watuhumiwa hao kuwa ni kulipa jumla ya N500,000 pamoja wadhamini wawili ambao ni ndugu wa damu.

Wadhamini hao pia wanapaswa kuweka dhamana ya akiba ya benki ya N100,000 kila mmoja.

Kesi iliahirishwa hadi Septemba 29 itakaposikilizwa tena mahakamani hapo.

Rais Aliyeupa Heshima Mchezo Wa Soka (Joao Havelange) Afariki Dunia
Dk. Tulia afunguka, asema Ukawa walimtukana tusi kubwa