Polisi katika kaunti ya Busia nchini Kenya wamemkamata mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 40 akisafirisha misokoto ya bangi aliyoificha kwenye begi na mingine kujizungushia mwilini.
Mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Albert Wabwire amekamtwa asubuhi ya Alhamisi katika eneo la Sio, akitembea kutoka Busia hadi Matayos nchini Kenya.
Polisi wanasema walipofanya upekuzi walimkuta akiwa na bangi kwenye begi alilokuwa amebeba huku kiasi kingine cha mzigo huo akiwa amefunga kwa magunia kuuzunguka mwili wake.
Mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Busia akisubiri kufikishwa mahakamani siku ya Ijumaa Desemba 31, 2021.