Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Yamungu Kayandabila amesema Benki Kuu ya Tanzania – BoT imejipanga kununua tani sita za Dhahabu kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya kuweka akiba katika mfumo wa fedha za kigeni.

Dkt. Kayandabila ameyasema hayo wakati wa semina kuhusu fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani katika sekta ya Madini mjini Geita na kuongeza kuwa wameanza kutekeleza utaratibu huo baada Bodi ya Wakurugenzi kutoa maelekezo ya kununua dhahabu.

Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Yamungu Kayandabila Akizungumza wakati wa Semina ya fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani Sekta ya Madini.

Amesema, “utaratibu wa kununua dhahabu na
kuihifadhi katika mfumo wa fedha za kigeni siyo mpya kwani uliwai kutumika mwaka 1990 na tunaifadhi fedha za kigeni kupitia dhahabu kwa kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yetu.”

Kwa upande wake Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha za kigeni BoT, Dkt. Anna Lyimo, amesema tayari BoT imenunua kilo 418 za dhahabu kutoka kwa wachimbaji Wadogo na Wakubwa, ikilenga kuzihifadhi katika mfumo wa fedha za kigeni.

Shughuli za kiuchumi kuchipuka upya mpakani Tanzania, Msumbiji
Tanzania, Saudi Arabia zajadili kukuza Utalii Nchini