Mwanaume mmoja raia wa Uholanzi amejikuta akilazwa hospitalini baada  ya kukaa katika Uwanja wa Ndege kwa siku 10 nchini China alipoenda kwa lengo la kukutana na mrembo aliyekuwa akiwasiliana naye mtandaoni, ambaye hakutokea.

Mtandaoni 2

Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Alexander Peter Cirk mwenye umri wa miaka 41, alisafiri kutoka Uholanzi na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changsha Huanghua kukutana na mrembo aliyemfahamu kwa jina la Zhang.

Hunan TV imeripoti kuwa Cirk alikataa kuondoka katika uwanja huo wa ndege, lakini hali yake ya afya ilizorota kwa kukosa maji ya kutosha na chakula, hivyo maafisa walilazimika kumkimbiza hospitalini.

Baada ya tukio hilo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari, mrembo huyo alijitokeza na kufanya mahojiano na Hunan TV wakati mwanaume huyo alikuwa tayari amesharushwa nchini kwao.

Zhang, mrembo aliyemtesa Cirk

Zhang, mrembo aliyemtesa Cirk

Mrembo huyo alieleza kuwa alidhani mwanaume huyo anatania pale alipomwambia anaenda nchini China kwa ajili yake. Aliongeza kuwa wakati wote huo yeye alienda kufanya upasuaji (plastic surgery), hivyo simu yake ilikuwa imezima.

“Siku moja alinitumia picha ya tiketi za ndege ghafla na nilidhani alikuwa anatania. Hakuwahi kuwasiliana na mimi tena baadae,” alisema mrembo huyo.

Hata hivyo, mwanaume huyo alipoulizwa wakati anarudishwa Uholanzi baada ya kutibiwa, alieleza kuwa anaamini atakaporudi nchini kwao wataendelea na uhusiano wao wa mapenzi mtandaoni.

Tundu Lissu aandika ujumbe akiwa mikononi mwa polisi baada ya kufanya mkutano
Raisi Magufuli Mgeni Rasmi Siku Ya Vijana Mkoani Simiyu