Klabu ya Azam FC imeendelea kufanya vyema katika soko la biashara ya kuuza wachezaji nje ya nchi, baada ya kuthibitisha nyota wake kutoka nchini Cameroon Alain Thiery Akono Akono, amepata dili la kwenda Malaysia.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo Thabit Zakaria (ZakaZakazi) amesema mipango ya mchezaji huyo ya kuondoka klabuni hapo inakwenda vyema na muda utakapowadia wataweka wazi anakwenda klabu gani.

“Mipango yote kuhusu kuondoka kwa Ankono Akono inakwenda sawa na kinachotakiwa ni mashabiki kuwa na subira ili kupata taarifa kamili ambazo tutazitoa hivi karibuni, ila ukweli ni kwamba amepata timu Malysia.”

Akono anakuwa ni mchezaji wa tatu kuuzwa kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Klabu ya Azam FC wengine ni pamoja na Novartus Dismas ambaye yupo Israel na Shaban Chilunda yupo zake nchini Morroco.

Akona alisajiliwa Azam FC Mwezi Agosti mwaka huu akitokea nchini kwao kama mchezaji huru kufuatia kumaliza mkataba wake Fortuna Du Mfou ya kwao.

Hatma ya Mdee na wenzake kufahamika Desemba 27
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 21, 2020