Kiungo Mpya wa klabu ya Simba SC amefichua siri ya kukubali kujiunga na klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Akpan alitambulishwa rasmi kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC jana Jumapili (Julai 10), baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili ndani ya Klabu hiyo ya Msimbazi.

Akpan amesema ukubwa wa klabu ya Simba SC na mapenzi ya Mashabiki wake, ndio sababu kubwa iliyomvutia kukubali kujiunganao, hivyo anaaamini ataweza kushinda mataji akiwa Msimbazi.

Amesema tangu alipowasili Tanzania kwa ajili ya kucheza soka alikua na ndoto za kuitumikia Simba SC kutokana na umahiri na ukubwa wa Klabu hiyo ndani na nje ya nchi, na leo ndoto zake zimetimia.

“Simba SC ni klabu kubwa sana Barani Afrika, kila mchezaji ana ndoto za kuitumikia klabu hii, binafsi nilitamani kuwa hapa siku moja, leo nimetimiza ndoto za kuwa sehemu ya kikosi cha klabu hii,”

“Mashabiki wa Simba SC wana upendo wa dhati, wamekua msaada mkubwa sana kwa wachezaji na timu yao inapokua kwenye majukumu ya kusaka ushindi, kwa hakika nitafurahia upendo wao kwa kipindi chote nitakachokua hapa.”

“Nipo tayari kufanya kitu kikubwa katika klabu hii, mimi ni mchezaji ninayetambua majukumu yangu, ninajua nini nitakachokifanya kwa kushirikina na wachezaji wenzangu kuanzia msimu ujao, sitawaangusha mashabiki wenye upendo wa Simba SC.” Amesema Akpan

Akpan amekua mchezaji watatu kutambulishwa Simba SC akitanguliwa na Mshambuliaji Moses Phiri kutoka Zambia pamoja na Mshambuliaji wa Tanzania Habib Kyombo aliyetambulishwa Jumamosi (Julai 09).

Simba SC kumtambulisha mwingine leo Jumatatu
Wanafunzi wafa kwa kukosa hewa ndani ya 'School Bus'