Kiungo wa kati wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Barcelona, Franck Kessie anakaribia kuhamia klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia, vyanzo vimeithibitishia.
Mchezaji huyo alijiunga na Barca kutoka AC Milan kwa uhamisho wa bila malipo msimu uliopita wa joto, na licha ya kufunga bao la ushindi la kukumbukwa dakika ya mwisho dhidi ya Real Madrid wakiwa njiani kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, La Liga, hakupewa nafasi nyingi zaidi pale Camp Nou.
Imeripotiwa kuwa Tottenham ilifanya mazungumzo na FC Barcelona juu ya kumsajili Kessie pamoja na mchezaji mwenzake, Clement Lenglet, ambaye alitumia msimu uliopita kwa mkopo kaskazini mwa London. Lakini Spurs watamkosa Kessie kwani amekubali kujiunga na Al Ahli.
FC Barcelona awali walidhani kwamba upendeleo wa Kessie ni kubaki Ulaya, lakini sasa watakaa chini na kuwapiku Al Ahli ili kupata Euro Milioni 15, ambao pia wamewasajili Edouard Mendy, Roberto Firmino, Riyad Mahrez na Allan Saint-Maximin katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya joto.
Kikubwa zaidi, FC Barcelona hawatalazimika kulipa sehemu ya mishahara ya Kessie ili kumwondosha kwenye vitabu vyao, hivyo kuwawezesha kubadilika zaidi chini ya vikwazo vikali vya kifedha vya Lliga.