Hivi karibuni Klabu ya Simba SC Tanzania ilipiga chini karibu ofa tatu za klabu ya Al Ahly wakimuhitaji kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Miquissone.

Wakati Simba wanapiga chini ofa za Al Ahly wakimuhitaji Miquissone, miamba hiyo soka ya Misri nayo imepiga chini ofa nne zilizowekwa mezani na miamba ya soka ya Uturuki, klabu ya Galatasalay ili kumsajili kiungo mkabaji wa klabu hiyo Aliou Dieng raia wa Mali.

Awali Galatasalay waliweka ofa ya Euro milioni 6.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 17.7 kwa pesa za Kitanzania, Al Ahly wakaipiga chini ofa hiyo.

Galatasaray kwasabau wana muhitaji sana nyota huyo wakaongeza mzigo ukafika mpaka Euro milioni 7 ambazo ni zaidi ya bilioni 19 kwa pesa za a Kitanzania lakini waarabu bado wakaendelea Kukaza, wakaipiga chini ofa hiyo tena.

Galatasaray hawakuchoka, wakatafakari wakaamua kuongeza mzigo tena , wakafika hadi Euro milioni 7.6 ambazo ni zaidi ya bilioni 20.7 kwa pesa za kitanzania yaani mzigo huu umezidi kidogo ule mzigo ambao Mo ameweka pale Simba lakini bado Al Ahly wakaitupilia mbali tena ofa hiyo.

Waliwaambia kuwa kama wana nia ya kumsajili Dieng watoe dau la Euro milioni 8 ambazo ni zaidi ya bilioni 21.8 kwa pesa za Kitanzania pia kwenye mkataba kuwepo na kipengele cha Al Ahly kupokea asilimia 20 ya mauzo iwapo nyota huyo atauzwa kwenda klabu nyingine.

Galatasary Bado hawajakata tamaa, wanatafakari na muda wowote kuanzia hivi sasa watarudi tena

Endapo Galatasalay watarudi na kutoa Euro milioni 8, basi Al Ahly watakuwa wamefanya biashara kubwa sana tena ambayo itakuwa imewalipa sana,

Kiasi hicho cha pesa kinaweza kutosha kuwasaidia Al Ahly kufanya usajili wao wote wa msimu huu ikiwemo kuwalipa Brighton Euro milioni 1.8 ambazo wanatakiwa kulipa ili kumpata nyota wa kimataifa wa Africa kusini Percy Tau.

Meneja afafanua uhalali wa Tuisila Kisinda
STAMICO,TANESCO waungana kuokoa rasilimali madini