Uongozi wa klabu ya Al Ahly umeuandikia barua uongozi wa chama cha soka nchini Misri (EFA), inayoelekeza hatua ya kukata rufaa yakupinga adhabu iliyotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) dhidi ya mshambuliaji wao Walid Azaro.
Mshambuliaji huyo ameadhibiwa kwa kutozwa faini ya dola za kimarekani 20,000 pamoja na kufungiwa michezo miwili, kufautia utovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa mchezo mkondo wa kwanza hatua ya fainali dhidi ya Esperance uliochezwa juma lililopita.
Kufautia adhabu hiyo Azaro atakosa mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa nchini Misri baadae mwezi huu, huku klabu yake ya Al Ahly ikiwa mbele kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja walioupata ugenini.
Uongozi wa Al Ahly umewataka viongozi wa EFA, kuwaomba CAF kutoa ufafanua wa kina kuhusu sheria iliyotumika kumfungia mshambuliaji huyo.