Uongozi wa Simba SC, umethibitisha siku ya kutua wapinzani wao, AI Ahly ambapo wameweka wazi kwamba watatua kesho Jumanne (Oktoba 17) wakitokea nchini kwao Misri.

Al Ahly wanakuja kucheza na Simba SC katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya African Football League, mchezo unaotarajiwa kufanyika Ijumaa (Oktoba 20), Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmedy Ally, amesema wageni wao hao wanatarajiwa kutua nchini kesho Jumanne (Oktoba 17), tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo baina yao.

“Al Ahly wanatarajiwa kutua nchini kesho Jumanne (Oktoba 17), tunaamini wanakuja kutafuta matokeo mazuri na sisi tuwaambie tu kuwa tupo tayari kwa ajili ya kuhakikisha timu yetu inapata matokeo mazuri dhidi yao.

“Mpaka wao wanacheza na sisi, basi wanatambua kuwa sisi ni timu kubwa na ya aina gani kwa kuwa mara zote wanatambua ukubwa wetu, hivyo wanakuja kwa adabu zote, lakini niwaambie tu sisi sio wanyonge na tutawaonyesha ukubwa wetu,”amesema kiongozi huyo.

Gamondi akemea ubinafsi Young Africans
Kiswahili chapigiwa chapuo Mikutano Benki ya Dunia, IMF