Wapinzani wa Simba SC, Al Ahly wameweka kiasi cha Tsh Billion 7 kwa ajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Dortmund na timu ya Taifa ya Ufaransa, Anthony Modeste.

Al Ahly inajipanga kukamilisha usajili huo katika dirisha hili la kiangazi, kufuatia Modeste mwenye umri wa miaka 35 kuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Dortmund kufikia ukomo.

Dortmund ilimsajili Modeste kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea FC Cologne mwanzoni mwa msimu wa 2022/23 kama mbadala wa Sebastien Haller kugundulika na tatizo la saratani ya tezi dume.

Msimu wa 2021/22 Mfaransa huyo aliifungia FC Cologne magoli 20, kabla ya kuitumikia Dortmund aliyoifungia mabao mawili.

Mshindi taji la Mtu mvivu kujinyakulia Mil. 2.6
Maxi, Zouzoua wakapewa kazi maalum Rwanda