Klabu ya Al Ahly ya Misri imemuuza jumla mshambuliaji wake raia wa Senegal, Aliou Badji, kwenda klabu ya Amiens SC ya Ufaransa inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Badji alijiunga na Al Ahly Januari 2020 akitokea klabu ya Rapid Vienna ya Austria kwa mapendekezo ya kocha wa wakati huo wa Al Ahly, Rene Weiler.

Lakini ujio wa Pitso Mosimane ukabadili hali ya hewa na kumfanya nyota huyo kuwa chaguo la nne nyuma ya Marwan Mohsen, Mohamed Sherif na Walter Bwalya.

Akatolewa kwa mkopo kwenda klabu ya ligi kuu ya Uturuki, MKE Ankaragücü.

Mkopo ulipoisha huko, akapelekwa tena mkopo kwenye klabu ya Amiens ya Ufaransa kukiwa na kipengele cha kuuzwa moja kwa moja kwa Yuro milioni 1.8.

Jamaa akakiwasha kwa kufunga mabao 13 na asisti 3 katika mechi 26, na sasa klabu hiyo imeamua kukitumia kile kipengele ili kumnunua moja kwa moja.

Walimnunua kutoka ligi kuu ya Austria, wakamtoa kwa mkopo ligi kuu ya Uturiki, na sasa wamemuuza moja kwa moja ligi daraja la kwanza Ufaransa kwa Yuro milioni 1.8, takribani shilingi bilioni 4 za Tanzania.

Na huyu ni mchezaji ambaye hana nafasi kwenye kikosi chao, yaani hatakiwi.

Try Again amkataa Saido Ntibazonkiza
Habari kuu kwenye magazeti ya leo June 5, 2022