Kiungo kutoka nchini Italia Marco Verratti amekamilisha usajli na kujunga na kikosi cha Al-Arabi cha Ligi Kuu ya Saudi Arabia, akitokea Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa dau la pauni milioni 45.

Verratti tayari alishashinda mataji tisa ya Ligi Kuu ya Ufaransa akiwa PSG tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2012, huku akiisaidia timu yake ya taifa ya Italia kubeba Kombe la Euro 2020.

Alisema amefurahia kujiunga na timu hiyo kwenda kutafuta changamoto mpya, hivyo ana matumaini ya kufanya vyema na kuhakikisha anaisaidia kufikia malengo ikiwemo kutwaa mataji.

“Ninajivunia kuvaa jezi ya PSG muda wote niliokuwa nao, nimekaa kwa kipindi kirefu katika kikosi hicho na nilikuwa ninaishi na wenzangu kama familia moja na tulipambana kuipatia heshima ya mataji mbalimbali.

“PSG ni moja ya timu zenye mashabiki wakutosha na ukarimu wao utabakia moyoni mwangu kwa kipindi kirefu zaidi.

“Nimefurahia kujiunga na AI-Arabi ni moja ya timu bora kwa sasa hapa Saudi Arabia, ninaamini nitaendelea kuisaidia kupata mataji zaidi,” alisema Verratti ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji wa Ulaya waliofanikiwa kujiunga na timu za Saudi Arabia.

MAKALA: Usichokijua kuhusu Barabara ya Shekilango
Miezi sita: Lokassa ya Mbongou bado hajazikwa