Mwendesha mashtaka mkuu wa nchini Sudani, Al-Waleed Ahmed, ameamuru kuhojiwa kwa Rais aliyeondoshwa Marekani, Omar al-Bashir, kwa tuhuma za utakatishaji fedha na kuhifadhili makundi ya ugaidi.
Shirika la habari la Sudan, SUNA, limesema kuwa mwendesha mashtaka huyo ameamuru mahojiano kufanywa chini ya sheria za kupambana na utakatishaji fedha na ugaidi.
Hatua hiyo inatokana na kukutwa na zaidi ya dola milioni 133 kwenye makazi yake ambazo alikuwa amezificha alipokuwa Rais wa nchi hiyo.
Al- Bashir aliingia madarakani kwa mapinduzi ya mwaka 1989 na kuiongoza Sudani kijeshi hadi mwaka huu alipoondolewa kwa shirikisho la umma.
Wakati wa utawala wake, Serikali ya Marekani iliiweka Sudani kwenye orodha ya wafadhili wa ugaidi kutokana na mahusiano yake na wanamgambo wa kundi la itikadi kali, akiwemo Osama bin Laden, ambaye aliishi huko kutoka mwaka 1992 hadi 1996.