Kikosi cha Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Hilal ‘Omdurman’ kimewasili mjini Pretoria, Afrika Kusini kikitokea Dar es salaam-Tanzania leo Jumanne (Februari 07).

Al Hilal ‘Omdurman’ iliweka Kambi ya majuma mawili jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa Kwanza wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns ‘Masandawana’.

Miamba hiyo itakutana Jumamosi (Februari 11) mjini Pretoria katika Uwanja wa Loftus Versfeld majira ya saa tisa alasiri kwa saa za Afrika Kusini.

Ikiwa nchini Tanzania Al Hilal ilicheza Michezo mitatu ya Kimataifa ya Kirafiki, ikiifunga Azam FC 1-0, na kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Namungo FC na Simba SC.

TFS yataka ushirikishwaji kupunguza gesi joto
Bishara ya Kaboni: Watanzania wahimizwa kupanda miti