Klabu ya Al-Ittihad baada ya kuona kuna ugumu wa kumpata, Mo Salah kutoka Liverpool sasa wanamtazama mshambuliaji wa Tottenham, Richarlison kama mbadala wa Salah baada ya dau lao la Pauni Milioni 150 kwa mshambuliaji wa Liverpool kukataliwa.

Richarlison aliripotiwa kuwindwa na klabu kadhaa za Saudi Pro League, huku Al-Itihad wakimtafuta mshambuliaji huyo katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili huko Mashariki ya Kati.

Mabosi wakuu wa Saudi Arabia walikuwa jijini London kwa mazungumzo na Liverpool na walikuwa tayari kulipa ada ya rekodi ya dunia kwa Salah, lakini Liverpool wakawakazia.

Gazeti la Telegraph limeripoti kuwa mshambuliaji wa Tottenham Richarlison anawindwa na klabu ya Al-Itihad.

Ilipobainika kuwa hawatampata Salah, upande wa Saudi ulitafuta njia mbadala, ripoti hiyo inasema.

Jadon Sancho kurudi Signal Iduna Park
Upanuzi wa migodi chanzo ukiukwaji haki za Binadamu