Wapinzani wa mabingwa wa Soka Tanzania Bara katika Raundi ya kwanza ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Young Africans, Al Merrikh ya Sudan wanasaka makali kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya hapa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Newstimes, timu hizo zitacheza Jumapili ya Septemba 3, 2023 ikiwa ni maandalizi ya mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Rayon inashiriki Kombe la Shirikisho.

Hata hivyo, bado mchezo huo haujajulikäna utafanyikia kwenye uwanja upi ambao umeandaliwa na Wilaya ya Nyanza kwa kushirikiana na FXB Rwanda kama sehemu ya kampeni ya kupambana na unyanyasaji na mimba za utotoni.

Al Merrikh kwa sasa imepiga kambi katika Wilaya ya Huye na imekuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Huye, ambao kwa sasa unatumika kama uwanja wa nyumbani wa timu hiyo kwa mechi za Ligi ya Mabingwa kutokana na vita nchini mwao.

Mabingwa hao wa Sudan walikuwa wenyeji wa AS Otoho ‘Oyo’ Ijumaa (Agosti 25) na waliitoa katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja huo kwa faida ya bao la ugenini na kutinga hatua inayofuata.

Kramo, Inonga mambo safi Simba SC
Marufuku kutuma nyaraka za Serikali kwa WhatsApp