Taarifa kutoka ndani ya Young Africans, zinaeleza kuwa Uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na wadhamini wao kampuni ya GSM, wamekubaliana kumpa ajira kocha kutoka nchini Tunisia Nasreddine Al Nabi.

Al-Nabi amekua akitajwa kutua Young Africans, baada ya Uongozi wa klabu hiyo kufuta ndoto za kumuajiri kocha kutoka nchini Ufaransa Sébastien Migné, ambaye alikua akitajwa kwa siku kadhaa zilizopita.

Al-Nabi anatarajiwa kuwasili nchini sanjari na kikosi kazi chake cha benchi la ufundi kitakachokuwa na watu watatu, ili kuiwezesha Young Africans kuwa na kikosi bora kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Inaelezwa kwamba Al-Nabi atakuja na Kocha MSAIDIZI wake wa kwanza, Mtaalam wa MAZOEZI ya viungo anayekuija kuchukua nafasi ya Mghana Edem Mortotsi ambaye ameshatimka nchini.

WASIFU WA KOCHA AL-NABI.

Kocha Nasreddine Al Nabi alizaliwa Januari Mosi, 1965, amezifundisha klabu mbalimbali ikiwamo Al Ahly Benghaz ya Libya aliyoinoa kati ya mwaka 2012-2013

Msimu uliofuata akatua Al Hilal aliyokaa nao kwa msimu mmoja wa 2013-2014 na kutwaa nao ubingwa wa Ligi Kuu ya Sudan na pia kuifikisha timu hiyo robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2014.

Kisha akatimkia Ismaily ya Misri aliyoinoa msimu wa 2015-2016 kwa kuchukua nafasi ya Mido, kisha kwenda Italia na kuiona Pont Donnaz Hone Arnad iliyopo Ligi Daraja la Nne msimu uliopita kabla ya kupewa ajira Al Merrikh kuanzia Januari 28 mwaka huu kuchukua nafasi ya Gomes aliyepo Simba.

Balaa kubwa likaja baada ya kuchukua nafasi ya Gomes aliweza kuisimamia timu hiyo kucheza mechi tatu tu za Ligi ya Mabingwa Afrika, akipoteza mbili dhidi ya As Vita na Al Ahly na kuambulia suluhu nyumbani dhidi ya wababe wa Kundi A, Simba na kufurushwa Machi 7, sambamba na wasaidizi wake.

Waziri wa TAMISEMI amsimamisha kazi Mkurugenzi Sengerema
Tetesi: Majukumu ya Zahera Simba SC