Wizara ya sheria nchini Libya imethibitisha kuachiwa kwa Al-Saad Gaddafi mtoto wa aliyekuwa Rais wa zamani wa Libya Moammar Gaddafi, kutoka gerezani baada ya kukaa Zaidi ya miaka saba.
Al-saadi ambaye ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu nchini Italia , alikuwa ameshikiliwa katika gereza la Tripoli kwa Zaidi ya miaka saba kutokana na kukabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya waandamanaji na mauaji ya kocha wa mpira wa miguu wa Libya Bashir Al-Rayani mwaka 2005.
Taarifa kutoka Libya zinaeleza kuwa kuachiliwa kwa Saadi Gaddafi kumetokana na mazungumzo ambayo yalikuwa pamoja na wakuu wa kabila,Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibeh na Waziri wa zamani wa mabo ya ndani Fathi Bashagha
Ripoti zinaeleza kuwa Saadi amesafiri kwenda nchini Uturuki baada ya kuachiwa huru.