Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab limedai kuhusika na mauaji ya ofisa mwandamizi wa upelelezi pamoja na mlinzi wake katika shambulio la barabarani huko kusini mwa Mogadishu.

Mohamud Moallim Hassan Qoley aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mchana katika wilaya ya Dharkaynlay, maafisa wa polisi wamesema kuwa Qoley alikuwa mkuu wa upelelezi katika eneo la Kahda moja ya wilaya 17 katika mji mkuu Mogadishu.

Ofisa huyo alikuwa pamoja na walinzi wawili wakati alipofyatuliwa risasi kwenye gari ambayo ilikuwa imejificha kwenye uchochoro ambapo mmoja wa walinzi alifariki papo hapo.

Aidha, wakati huo huo wanajeshi wanne wa serikali waliuwawa baada ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab kushambulia kituo kimoja cha ukaguzi cha jeshi katika mkoa wa Hiran uliopo kaskazini mwa Mogadishu.

Hata hivyo, Wanamgambo hao walifanikiwa kuchukua silaha kutoka kwa wanajeshi kwenye kituo cha ukaguzi kwenye barabara kuu inayounganisha Somalia na Ethiopia

Familia ya Lissu yatoa ya moyoni kuhusu dereva wake
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 18, 2017