Ripoti ya taasisi ya Hiraal yenye makao yake mjini Mogadishu inasema kundi la al-Shabab nchini Somalia lilitumia dola milioni 24 ambazo ni zaidi ya bilioni 55 za kitanzania mwaka 2021 kununua silaha.
Ripoti hiyo pia inadai kuwa kundi la al-Shabab, ambao hufungamana na al-Qaeda, inakusanya mapato ya karibu dola milioni 180 kila mwaka.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la ‘Al-Shabab’s Arsenal-From Taxes to Terror’, inasema kundi hilo linatumia mbinu mbalimbali kupata silaha, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa moja kwa moja kutoka soko la ndani, na kutoka kwa wafanyabiashara wa silaha walio na kandarasi ya kununua na kusambaza silaha kutoka nje ya nchi, hasa Yemen.
Taasisi ya Hiraal pia imesema kwamba waasi wanadhibiti sehemu kubwa ya Somalia na kudumisha kiwango cha ushawishi kwa raia kupitia mchanganyiko wa ushawishi, utawala na kulazimisha.