Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amepitia upya mipango yake ya usajili na sasa anajiandaa kurudi tena sokoni kutatua tatizo la safu ya ulinzi linaloikabili klabu hiyo ya Anfied.

Mkuu huyo wa benchi la ufundi la majogoo wa jiji wakati akiwa na timu yake mjini Los Angeles Marekani, alionesha kwamba baada ya kusajili wachezaji saba, biashara yake ya usajili imekwisha, ingawa alishindwa kumpata mlinzi wa kushoto wa mabingwa wa EPL, Leicester City, Ben Chilwell.

Klopp kwa sasa emepanga kumtumia James Milner kama beki wa kushoto kwa dharura, baada ya kuona mchezaji wa nafasi hiyo ambaye ni chaguo la kwanza Alberto Moreno akiumia kwenye mchezo waliopoteza dhidi ya AS Roma, amethibitisha kuingia sokoni kama mchezaji anayemhitaji atakuwepo.

Liverpool ina majeruhi kama Mamadou Sakho, Joe Gomez na Joel Matip  ambao wote ni walinzi wa kati, wakati  Lucas Leiva, ambaye anaweza kuziba nafasi hizo naye anaendelea kuimarika kutokea kwenye majeraha ya nyama za paja.

Hata hivyo Liverpool bado wanaendelea kuhusishwa na mpango kumsajili beki wa Cologne, Jonas Hector kwa dau la Pauni milioni 20.

Chelsea Wabuni Mbinu Mpya Ya Kumrejesha Lukaku
Azam FC Kujipima Kwa Maafande Wa JKT Ruvu