Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba amefunguka sababu za album yake kuhusisha idadi kubwa ya wasanii wenye majina makubwa na wasanii chipukizi wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva.

Nyota huyo, ni Star mwenye uwezo wenye kujitosheleza kiasi cha kuweza kusimama mwenyewe na kufanya mradi unaoweza kufika mbali, kutokana na ukubwa wa talanta pamoja na uzoefu alionao kwenye kiwanda cha muziki huo.

“Nilivyokuwa na wazo la album nilimpelekea Nassib (Diamond Platnumz) nikamwambia mimi nataka kufanya album, yeye ndio aliniambia kwamba, bwana hauna namba za digital platforms, muziki umetoka kwenye sehemu ya burudani sasa hivi ni biashara,” amesema Barnaba.

Amefafanua kuwa, “Kwa hiyo kama unaona digital ndio cha kufanya ndugu yangu ni lazima tutafute wasanii wenye namba, mimi mwenye nitakuwa wa kwanza, tafuta wengine, muweke na Ali Kiba hii cheketua bado inafanya vizuri, tafuta na wengine kadhaa.”

Aidha, Barnaba amongeza kuwa “Usisahau sisi tunakimbia tushavuka, new generation wana namba kuliko sisi kwa sababu ni watu wanaochipukia na wanabaki hapo, kwa sababu wana miaka mitatu minne ya kuendelea kufanya vizuri hivyo waweke.”

Barnaba anaendelea kuwa, “So wazo lilikuwa la kwake na nikaona ni zuri lakini kiukweli nimefanikiwa kwasababu ukifuatilia ngoma zinazofanya vizuri kwenye stream pale utakuja kugundua kuwa new generation wanafanya vizuri, sisi tunafanya vizuri sana lakini ngoma nilizofanya na wasanii wapya zimekuwa kubwa kuliko hata unavyofikiria.”

Pamoja na kuweka wazi, kuhusu lilipotokea wazo la yeye kushirikisha idadi kubwa ya wasanii chipukizi kwenye kiwanda cha muziki nchini, pia nyota huyo amedokeza sababu ya album hiyo kukosa kabisa wimbo hata mmoja ambao ameimba yeye peke yake.

Hata hivyo, Barnaba amesema huo ulikuwa ni wakati sahihi wa yeye kushiriki na wasanii tofauti tofauti kwenye kazi zake kutokana na kuwa si msanii ambaye amewahi kufanya kazi na wasanii wengi ukiachilia mbali nyimbo kadhaa zilizowahi kufanya vizuri alizoshirikiana na wasanii kama Ray C, Linah Sanga, Amini n.k.

Love, Sounds, Different album iliachiwa rasmi Aust 16, 2022 ikiwa ni album ya tano ya nyota huyo, baada ya Refresh Mind, Kichwa Changu, Gold, Ambient Noised State (Missed White Noised Idea) pamoja na Mapenzi Kitabu.

Tanzania na Msumbiji kuondoa vikwazo vya Kibiashara
Ajenda ya DC Kisarawe yaungwa mkono kwa ujenzi Chuo cha Ufundi