Drake ameonesha dunia kuwa yeye ni kati ya marapa bora zaidi duniani kwa sasa ingawa amekutana na changamoto za beef kati yake na Meek Mill.

Kanda Mseto yake (mixtape) aliyoiachia ghafla, ‘If You’re Reading This It’s Too Late’ imefikisha mauzo ya platinum na kuwa ya kwanza kati ya Album zilizotoka mwaka huu, kufikia mauzo hayo. Mixtape hiyo imeuza zaidi nakala zaidi ya 52,000  ndani ya wiki hii hivyo kufanya mauzo ya jumla kufikia milioni 1.007 katika mauzo ya dijitali.

Mauzo hayo ya Drake yamefanyika kupitia teknolojia ya dijitali bila kuhusisha mauzo ya nakala zinazoshikika (physical copies).

Taarifa hizi sio nzuri kwa hasimu wake Meek Mill ambaye hivi karibuni alidai kuwa Drake hana uwezo wa kuandika mistari yake mwenyewe.

Hamfrey Polepole, Mchungaji Msigwa Wakabana Kuhusu Lowassa Na Ukawa
Lowassa Awavuta Boda Boda, Machinga Na Mama Ntilie