Gwiji wa klabu ya Liverpool, John William “Aldo” Aldridge ameshangzwa na mpango wa Man Utd kuwa katika harakati za usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Juventus, Paul Pogba.

Aldridge ambaye ni raia wa England, ameshangazwa na mpango huo, kutokana na kuamiani Pogba sio mtu sahihi wa kusajiliwa na klabu hiyo kwa kigezo cha kiwango chake, ambacho kimekua gumzo tangu alipoanza kuhusishwa na mipango ya kurejea Old Trafford.

Gwiji huyo amesema itakua ujinga na upuuzi kwa Man Utd, kama watakamilisha usajili wa kiungo huyo, tena kwa ada ya uhamisho inafikia Pauni milion 100 ambayo imetajwa na uongozi wa Juventus.

“Kama soka limefikia hatua ya kuongozwa na vichaa, jambo hilo litatokea kwa Pogba na sitoshangaa, kwa sababu sioni kinachowafanywa Man Utd kujiingiza kwa Pogba tena kwa ada kubwa ya usajili ya Pauni milion 100,” Aldridge alimueleza mwandishi wa gazeti la Sunday World.

“Pogba ni mchezaji wa kawaida, wala hakunishawishi kumtazama mara kwa mara alipiokua katika michezo ya Euro 2016, ninasikitishwa na taarifa za Man Utd kuwa mstari wa mbele kuhitaji kuwa nae kwa msimu ujao wa ligi ya England.

“Kama Man Utd watanifuata na kunitaka ushauri nitawaambia hivyo bila kufucha, na endapo wanahitaji mchezaji wa kumsajili kwa ada itakayovunja rekodi ya dunia ni bora waanze mpango wa kumshawishi Cristiano Ronaldo ama Lionel Messi, ambao wanye thamani ya Pauni milioni 100 katika kipindi hiki.” Alisisitiza Aldridge aliyeitumikia Liverpool kuanzia mwaka 1987 hadi 1989.

Renato Sanches Mchezaji Bora Euro 2016
Jambazi aliyetoroka Mwanza aibua hofu, Wizi wa fedha za Umma SMZ ni kigugumizi