Mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu bingwa nchini Italia, Juventus, Alex Sandro Lobo Silva ameonyesha azma ya kutaka kuondoka Juventus Stadium ili akatafute maisha mbele ya safari katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Sandro ameweka dhamira hiyo kwa kusema angependa kujiunga na klabu ya Man city ya nchini England, ambayo ni sehemu ya timu zinazowania nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

“Nina malengo ya kutimiza ndoto ya kwenda kucheza katika Ligi ya premier.” “Ninataka kuona ninalinda kipaji changu, sitaki kuwa msiri juu ya mimi kuondoka hapa.” “Soka ni kazi ninayokwenda kufanya popote, soka ni mchezo wa kuangalia leo na kesho, huu ndio msimamo wangu kwa sasa,” alisema Sandro mwenye umri wa miaka 24.

“Manchester City ni klabu ninayoipenda kwa ajili ya soka langu la baadae, ninaamini nina nafasi ya kucheza nikiwa kule na kutimiza ndoto yangu hii,” alisisitiza Sandro raia wa Brazil.

Luis Suarez Ampuuza Andon Zubizarreta
Bafetimbi Gomis Kurejeshwa Nyumbani Na PSG