Klabu ya Rubin Kazan ya Urusi imemsajili kiungo wa kutoka nchini Cameroon, Alex Song ambaye alikuwa huru.

Hata hivyo, tangazo la usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 katika tovuti ya klabu hiyo halijaeleza kwa kwa undani juu ya mkataba aliousaini.

Song ameitumikia timu ya taifa ya Cameroon katika michezo 49, na kwa upande wa klabu amewahi kupita Arsenal, FC Barcelona pamoja na West Ham Utd.

Kiungo huyo aliibukia kwenye kikosi cha Arsene Wenger baada ya kujiunga na The Gunners kwa mkopo mwaka 2005, na akacheza mechi zaidi ya 150 katika klabu hiyo kabla ya kwenda Hispania mwaka 2012.

Hata hivyo, akiwa Fc Barcelona alishindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza, hatimaye akatemwa baada ya kucheza mechi 65 tu za mashindano yote ndani ya miaka minne.

Kiungo huyo mkabaji pia alicheza kwa misimu miwili kwa mkopo West Ham baada ya kushindwa Barcelona.

Mwishoni mwa mwezi Mei, meneja wa zamani wa Malaga, Javi Gracia aliajiriwa na klabu ya Rubin Kazan kama mkuu wa benchi la ufundi, kufuatia kumaliza nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Urusi na ndiye anayemsajili Song.

Mandanda Amkimbiza Alex McCarthy Selhurst Park
Liverpool Yaangukia Pua, Yapigwa 2-1