Klabu ya Villarreal ya nchini Hispania, imethibitisha kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Alexandre Pato.

Villarreal wamekamilisha usajili wa mshambuliaji huyo ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alisajiliwa kwa mkopo na klabu ya Chelsea ya nchini England akitokea Corinthians.

Taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya klabu hiyo ya El Madrigal zimeeleza kuwa, Pato amesaini mkataba wa miaka minne.

Hata hivyo haikuelezwa ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kama ada ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye aliwahi kutamba na klabu ya AC Milan ya nchini Italia kuanzia mwaka 2007–2012.

Klabu ya Sevilla CF ya nchini Hispania, nayo ilikua inahusihwa na mpango wa kutaka kumsajili Pato.

Pep Guardiola Ampiga Kibuti Vincent Kompany
Francis Coquelin Kuziba Nafasi Ya Per Mertesacker