Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia umuhimu wa suala la elimu.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo baada ya sala ya ijumaa katika msikiti wa Abuu Ubadya uliopo Fuoni Meli Saba Mkoa wa Mjini Magharibikuwataka wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma elimu zote mbili ikiwemo elimu ya dini na elimu ya dunia, kufanya hivyo itasaidia kuharakisha hatua za kimaendeleo.
Amesema mataifa yaliyoendelea kwa kiasi kikubwa wamewekeza fedha nyingi kwenye elimu ya utafiti kutokana na kuwa elimu ndio inayoleta mafanikio.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia ameongeza kuwa, moja ya sababu kuu za mmomonyoko wa maadili katika jamii hutokana na ukosefu wa elimu.