Mwimbaji wa ‘Chekecha Cheketua’, Ali Kiba ameelezea mpango uliowahi kuwekwa wazi na Davido mwaka 2015 kuwa kuna collabo inafuata kati yake na mkali huyo.

Akiongea na Ayo TV, Ali Kiba alieleza kuwa Davido ambaye alimtambulisha Diamond kimataifa kupitia collabo yake ya ‘Number One Remix’, ndiye aliyekuwa anatamani kufanya naye kazi.

King Kiba alieleza kuwa yeye na Davido sio washikaji lakini uongozi wake ndio uliofanya mawasiliano na mkali huyo wa ‘Fan Me’ na kuhusu uwepo wa collabo hiyo.

Ingawa anasema hakuwahi kuongea na Davido hapo kabla, hivi sasa Davido anataka wakae pamoja na kutengeneza kitu kizuri kwa ajili ya mashabiki wao.

 

 

Ni Mzunguuko Wa Tatu Wa Kombe La Shirikisho
Justin Bieber aeleza Kwanini Hataweza tena kuwa na Selena Gomez

Comments

comments