Ali Kiba amefuta video ya wimbo wake mpya ‘Hela’ kwenye akaunti yake ya YouTube, saa chache baada ya kuuachia rasmi.

Video ya wimbo huo ilivuta mjadala mrefu kwenye akaunti yake, wengi wakieleza kuwa sio wimbo mpya na kwamba umewahi kusikika miaka kadhaa iliyopita.

Hela ni wimbo uliokuwa unazungumzia jinsi ambavyo fedha zimekuwa kikwazo na chanzo cha matatizo mengi ikiwa ni pamoja na rushwa inayowanyima haki watu masikini wanapohitaji huduma muhimu.

Bado haijafahamika sababu hasa ya kufuta wimbo huo kwenye YouTube, kakini inasadikika kuwa ‘comments’ hasi za mashabiki wengi zinaweza kuwa chanzo.

Ali Kiba na Menejimenti yake hawajazungumzia sababu rasmi za kuchukua hatua hiyo hadi sasa.

Huu ni wimbo wa pili kwa Ali Kiba kuwa na misukosuko YouTube. ‘Mvumo wa Radi’ ulipata msukosuko wa dukuliwa na kusababisha idadi ya watu wanaotazama kuwa inashuka badala ya kuongezeka.

Athari 11 za kuongeza matiti
Video: Maajabu ya vikongwe kujifungua watoto