Mkurugenzi wa Kings music mwanamuziki Ali Kiba ni miongoni mwa wasanii walipata nafasi ya kushiriki kwenye album mpya ya nyota wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones ambayo ameachia rasmi leo Machi 7, 2022.

Kiba ameshirikishwa kwenye wimbo namba tisa  uitwao ‘Wanguvu’ unaopatikana kwenye album hiyo ‘Invisible Currency’ yenye jumla ya nyimbo 17.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa twitter Ali Kiba amempongeza Khaligraph ikiwa ni pamoja na kudhihirisha kiwango cha furaha aliyonayo juu ya ushiriki wake katika album hiyo.

“Congratulations Papa Jones, happy to be part of this project !!! Track No.9 !! GO STREAM THE ALBUM OUT NOW. #InvisibleCurrency,” ameandika Kiba.

Hii si mara ya kwanza kwa Ali Kiba kusikika kwenye wimbo mmoja na rapa Khaligrah Jones, ikumbukwe kupitia album ya ‘Only One King’ pia Kiba alimshirikisha rapa huyo kwenye wimbo ‘Habibty’.

Drake aliwa milioni 645 kwa ku-bet
Matola afichua siri ya kuibanjua Dodoma Jiji FC