Safari ya Ali Kiba kuelekea level za kimataifa imeonesha ‘taa ya kijani’ tayari ambapo anatarajia kufanya wimbo na mkali wa RnB toka Marekani, Ne-Yo.

Kampuni ya RockStar4000 imetangaza habari hiyo kupitia Instagram, habari ambayo imeibua shangwe zaidi kwa mashabiki wa Ali Kiba kwenye mtandao huo.

“Exciting News: African superstar Alikiba will be collaborating with International Superstar Ne-Yo; More news to follow #kingkiba #ROC.” Wameandika RockStar4000.

Ne-Yo atakutana na Ali Kiba kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio nchini Kenya hivi karibuni. Msanii huyo anakuwa msanii wa pili wa Marekani kufanya kazi na Ali Kiba ambapo miaka kadhaa iliyopita, R-Kelly na Ali Kiba waliimba pamoja kwenye wimbo maalum wa ‘One8’ uliwashirikisha wasanii wengi wakubwa Afrika, Hands Across The World.

Siku kadhaa zilizopita kwenye tuzo za MTV/MAMA, Ne-Yo alimtaja Diamond Platinumz kuwa msanii wa Afrika anayemkubali zaidi na kuna mpango wa kufanya kazi pamoja.

Habari hii ya Ali Kiba na Ne-Yo inaongeza nguvu zaidi kwa wadau wa muziki nchini kuamini kuwa Tanzania ina vipaji vingi vikubwa vinavyoweza kufika level ya kimataifa na kufanya vizuri.

 

Octopizzo Ashindana Na Dr. Dre, Ashangaa ‘Sheng’ Ilivyotusua
Ni Ronaldo, Messi Na Suarez 2015